Mfalme wa mwituni Simba ,atarejea Rwanda kwa mara ya kwanza tangu aangamie wakati wa mauaji ya kimbari mwaka wa 1994
Maafisa wanaowalinda wanyama pori wa Rwanda, wanasema kuwa simba watarudi nchini humo siku ya jumatatu kwa mara ya kwanza, tangu walipoangamizwa baada ya mauaji ya kimbari,ya mwaka wa 1994.
Simba wawili dume, na majike watano, wanasafirishwa kutoka mbuga ya wanyama ya Kwazulu Natal, Afrika Kusini, na Jumatatu watawasili Rwanda kwa ndege.
Simba hao saba watawekwa kwenye karantini kisha waruhisiwe kutembea huru katika mbuga ya wanyama.
Wanyama hao watapelekwa katika mbuga ya taifa ya Akagera.
Maafisa wakuu huko Rwanda walisema, kurejeshwa tena kwa simba nchini Rwanda ,ni Kilele cha juhudi kubwa ya kuhifadhi mazingira katika mbuga hiyo na kwa taifa zima kwa jumla.
Baada ya mauaji ya kimbari mwaka wa 1994, watu wengi waliokimbia makwao waliikalia mbuga hiyo ya Akagera.
Simba waliokuwa humo walikimbia au kuuawa, huku watu wakijaribu kulinda mifugo yao na maisha yao.