Skip to main content

Posts

Kiboko wa Bongo Movies Ney wa Mitego Ajichora Tatuu Mwili Mzima

Kwenye stage ya SERENGETI FIESTA 2012 msanii wa bongofleva Ney wa Mitego alivua t-shirt yake na kuacha mwili wake kuonekana mbele ya maelfu ya watu waliohudhuria ambapo michoro miwili mikubwa ilionekana kifuani kwake na mgongoni, michoro ambayo wengi waliyoiona walitamani kufahamu sababu za yeye kujichora hivyo. Ney amesema “tattoo yangu ya kwanza niliichora nikiwa darasa la saba so napenda tattoo, mi napenda maisha flani hivi ya kihustler unajua… huyu jamaa kifuani nimemchora ni wale mamafia, masniper nawapenda na hakuna maana nyingine zaidi ya hiyo” Kuhusu huu mchoro mgongoni mwake, Ney amesema “mi napenda mafuvu sana hata ukiingia ndani kwangu kuna picha nimebandika za mafuvu ukutani sielewi kwa nini huwa nazipenda”

Waziri Magufuli Awatia Adabu Wachina

KAMPUNI ya Kichina ya Chico imeanza kubomoa na kujenga upya kipande cha barabara ya lami kati ya Shelui na Mlima Sekenke, mkoani Singida chenye urefu wa zaidi ya kilomita 33. Akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Singida baada ya kukagua eneo hilo jana, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alisema kampuni hiyo inatakiwa kubomoa na kujenga upya kipande hicho kwa gharama zake yenyewe, baada ya uchunguzi uliofanywa kuonyesha ujenzi ulifanyika chini ya kiwango. Dk Magufuli alisema barabara hiyo iliyojengwa kwa zaidi ya Sh35 bilioni mwaka 2008 zikiwa mkopo, ilitarajiwa kudumu kwa zaidi ya miaka 15 lakini imebomoka kipindi kifupi. Dk Magufuli alisema serikali imechukua hatua hiyo ili kutoa fundisho kwa kampuni nyingine zinazoteleleza miradi chini ya kiwango na kusababisha hasara kwa Watanzania. Alitoa onyo kwa makandarasi washauri na wahandisi wanaopewa jukumu la kusimamia miradi hiyo, kuwa makini. Kwa mujibu wa mkataba ujenzi huo unatarajiwa kukamilika kabla ya Januari...

FIESTA YA DAR ILIVYOFANYIKA NA THE BOSS

     Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Rick Ross akiimba jukwaani  usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake kwenye viwanja vya Lidaz Club,wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likirindima.  Mkali mwingine wa miduara AT na madansa wake wakilishambulia jukwaa.  Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,akiimba jukwaani na shabiki wake.  Mashabiki wakitaka kuangusha uzio uliowekwa kwa ajili ya usalama.  Baadhi ya Askari wakijaribu kuweka usalama wa kutosha kwa Mwanamuziki Rick Ross imara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Lidaz Club,kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 201.  Viwanja vya Lidaz palikuwa hapatoshi hata kidogo.  Mwanamuziki kutoka nchini Marekani,Rick Ross akijisikia furahaa kuwaona Watanzania wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumshuhudia yeye akikamua stejini. Watu kibao wakiwa ndani ya viwanja vya lidaz...

K-LYINN AJIFINGUA MAPACHA

Aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Jackline Ntuyabaliwe aka K-Lynn amejifungua watoto mapacha. Kwa mujibu wa vyanzo, K-Lyinn amejifungua mapacha wa kiume wenye afya njema. Mpekuzi  inampongeza Jackline kwa kujifungua salama

FUKWE ZAFUNGWA AFRIKA KUSINI KUFUATIA KUVAMIWA NA PAPA WEUPE WALIOKUWA WAKINYATIA MZOGA WA NYANGUMI.

 Wafanyakazi wa mamlaka ya Usalama wa baharini nchini Afrika Kusini wakiwa katika harakati za kusogeza mzoga wa Nyangumi nchi kavu kwa ajili ya kwenda kuzika.   Sehemu kubwa ya pwani ya Afrika Kusini imefungwa kufuatia mzoga wa nyangumi mwenye ukubwa wa mita 30 kusukumwa na maji pembezoni mwa fukwe na kuanza kushambuliwa na jamii ya papa weupe.   Mzoga wa nyangumi huyo umelazimika kuondolewa haraka ufukweni ulikokuwa ukielea, kwa kuwa ulikuwa ukifukuziwa na papa weupe kadhaa walio ugeuza kitoweo na kuhatarisha maisha ya watu.   Mamlaka husika zimechukua hatua ya kuuondoa mzoga huo lakini pia imefunga mtandao wa fukwe hizo kuanzia Muizenberg hadi Monwabisi kwa tahadhari. Mzoga wa Nyangumi ukipimwa urefu.  Mashine Maalum ya kubebea vitu vizito kama Makontena ikifanya kazi ya kusomba mzoga huo. Jitihada za kumbeba Nyangumi huyo kwa kutumia mashine maalum za kubebea mak...