Skip to main content

Posts

Jokate Aoga Mvua ya MATUSI Toka kwa Mashabiki

Mwanamitindo  na Msanii wa Bongo Fleva, Jokate Mwegelo, maarufu kama ‘Kidoti’ amejikuta akiambulia matusi ya nguoni kwa kosa la kumpongeza msanii mwenzake wa Bongo Fleva, Ali Kiba baada ya kutwaa tuzo tano za Kili Music Awards zilizotolewa mwezi huu jijini Dar. Mwanadada huyo ameioga mvua hiyo ya matusi katika akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Intagram kwa watu tofauti kwa kile kilichodaiwa kuwa anahaha baada kuachwa na Mbongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ ambapo ameamua kufanya hivyo ili kuupoza mtima wake na kwa sasa kuna taarifa kwamba Ali Kiba ndiye anayemmiliki mtoto huyo.   Baada ya kutokea ishu hiyo, Mwandishi alimtafuta Jokate ili kusikia anazungumziaje hilo ambapo alisema:  “Nashindwa kuielewa jamii inataka mtu aishi vipi, lakini yote kwa yote siwezi nikamkandia mtu kwenye muziki wake, kwa upande wangu mimi ni shabiki wa Ali Kiba kwa sababu ninapenda kazi zake na hakuna wa kunizuia kufanya chochote juu yake.”

Hapatoshi CCM Dodoma

Fundi akisugua ukuta kabla ya kuanza kupaka rangi makao makuu ya CCM mjini Dodoma jana ikiwa ni matayarisho kwa ajili ya vikao vya kamati ya maadili, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya chama hicho vitakavyo kaa mapema mwezi ujao kwa ajili ya kuteua majina ya wagombea kuteuliwa kugombea urais kupitia chama hicho.  Dodoma. Kumekucha na Hapatoshi mjini Dodoma. Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea hali ilivyo mjini hapa, wiki mbili kabla ya vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanza kazi ya kumtafuta mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba. Hekaheka za maandalizi ya vikao hivyo kuanzia vya maadili, Sekretarieti, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa, zimeanza kuonekana wazi huku nyumba zote za kulala wageni na hoteli zikiwa zimekwishajaa kwa muda wote wa vikao hivyo. Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi kwenye maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma, umebaini kuwa nyumba za kulala wageni na hoteli zimejaa kuanzia Julai 8 hadi 12, mwaka huu. ...

IS yarejea kwa kishindo Kobane

Mshirikishe mwenzako IS yarejea kwa kishindo Kobane Ripoti kutoka Syria zasema kuwa wapiganaji wa Islamic State wamerejea katika mji wa Kobane. Wapiganaji hao wamerejea kwa mara ya kwanza tangu washambuliwe na muungano wa wapiganaji wakurdi . Tayari watu kadha wameripotiwa kufariki katika mpaka baina ya Uturuki na Syria. Jaribio lla kuteka miji ya Kobane na Hassakeh ni ilani kwa ulimwengu kuwa huenda wapiganaji hao wamepata nguvu mpya. Kundili la wachunguzi wa Human Rights limesema vita hivyo vilianza baada ya bomu lililokuwa limetegwa kwa gari kulipuka katika eneo la kuvukia. Mji huo wa Kobane uliharibiwa pakubwa baada ya vita vilivyoongozwa na Wakurdi kwa muungano na Marekani Wapiganaji wa Kikurdi wanaoungwa mkono na jeshi la Marekani linaloongoza mashambulizi ya angani walikuwa wameteka mji huo wa Kobane katika tukio lililoonyesha ushindi mkubwa dhidi ya IS. Kuna taarifa kuwa wapiganaji wa Islamic State waliingia mji wa kaskazini Hasake na kuteka maeneo mawili yalio...

Shamsa Ford: Dickson (ex wake) amewahi kunitishia kutuua mimi na mtoto zaidi ya mara 10

Muigizaji wa filamu, Shamsa Ford amesema tangu aachane na aliyekuwa mume wake Dickson Matoke, amewahi kuwatishia kuwaua yeye na mwanae zaidi ya mara 10. Shamsa alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV kuwa ex wake huyo alikuwa na matatizo mengi ambayo alishindwa kuyavumilia.   “Namshukuru baada ya kuwa gizani sasa hivi nipo kwenye mwanga. Dickson kanifanya nijifunze vitu vingi sana, vitu vingi vya kifamilia nilikuwa nafanya mimi kama mimi, yeye kazi yake ni kukesha baa anakunywa pombe na marafiki zake.Nimeshagombana na marafiki zake wote,”  Shamsa alimwambia mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema.   “Kuhusu kumtaka mtoto huo ndo ugomvi wetu huwa tunagombana kila siku. Sababu ya kwanza kwanini namnyima mtoto wangu Dickson alishaonyesha roho mbaya kwa mtoto wangu na mwanamke yoyote ambaye una uchungu na mtoto wake huwezi kumuachia mtoto.    "Dickson alitamka sio mara moja, siyo chini ya mara kumi, katamka kwangu, mbele ya ndugu zake...

VIDEO YA WIMBO MY TOWN YA WIZ MMS SOON ANGALIA PICHA HAPA!!!!

new hit soon itakua masikioni mwako mtu wangu nyimbo inaitwa  Huddah Monroe The Boss Lady love song eti  Huddah The Boss Chick  will you be mine? hahahahahahahahaahahahahahahahahah kind off

Master Mkwasa atambulishwa rasmi

Mshirikishe mwenzako Mkwasa atambulisha rasmi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemtambulisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya TanzaniaCharles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari. Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha hao wazawa wanaoanza kazi kesho kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala. Mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, kocha Mkwasa amesema anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi hiyo ya kuingoza Taifa Stars na msaidizi wake Hemed Morocco, na kuomba watanzania kuwapa sapoti. Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili. Aidha Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya ...