Kuzimwa kwa mitambo ya kurushia matangazo ya televisheni kwa mfumo wa analojia, kumezua utata baada ya wakazi wengi wa Mkoa wa Dar es Salaam kushindwa kupata matangazo. Mitambo hiyo ilizimwa juzi usiku kwa maelekezo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, wamesema hawapati matangazo ya televisheni licha ya kununua ving’amuzi. Aidha, wamesema chaneli tano zilizopewa leseni na serikali kuendelea kurusha matangazo yao, nazo zinaonyesha chenga chenga. Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili jana, walidai kuwa mfumo huo umeleta usumbufu mkubwa kwao. “Mimi mwenyewe nimekumbwa na tatizo hili tangu jana baada ya mitambo hiyo kuzimwa, sipati tena zile chaneli tano ambazo serikali ilisema ni lazima zionyeshwe ili Watanzania waendelee kuona hata kama vocha zao zitakuwa zimekwisha,” alisema mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam, ambaye hata hivyo, hakutaka jina lake liandikwe gazetini. Alidai kwamba kituo cha TBC tu ndiyo kilikuw