Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu hali ya vurugu zinazoendelea Mtwara katika sakata la mradi Gesi asilia kuja Dar es Salaam.PICHA NA VENANCE NESTORY Na Neville Meena, Mwananchi Dodoma: Wabunge Wawili Maarufu wa Chadema, Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini) na Godbless Lema (Arusha Mjini) wameingia katika vita ya maneno ambayo chanzo chake ni kauli ya Lema aliyotoa katika kikao cha wabunge (briefing) kilichofanyika mjini Dodoma Jumanne wiki hii. Lema akizungumza katika kikao hicho, anadaiwa kutoa maneno ambayo yalitafsiriwa na wabunge wengi kuwa yalikuwa yakimlenga Zitto kuhusu hatua yake ya kukataa posho na kumtuhumu kwamba ana ukwasi ambao unapaswa kuhojiwa. Gazeti hili lilimtafuta Lema likirejea taarifa iliyotolewa na Zitto akilalamika kwamba Lema alimshambulia katika kikao hicho cha wabunge wote na kwamba alikuwa akimlenga yeye. Lema, hata hivyo, alikiri kuzungumzia suala hilo akise