Skip to main content

Posts

CHAMPION LEAGUE PLY OF ROUND

Arsenal yaichapa Fenerbahce 3-0

Jack Wilshere mbele na Raul Meireles wakipambana Walipua mizinga wa Kaskazini mwa London, Arsenal wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya hatua ya makundi. Arsenal iliyokuwa ugenini huko nchini Uturuki imeichapa Fenerbahce nyumbani kwao 3-0 katika mchezo ambao ulishuudia kipindi cha kwanza kikimalizika bila nyavu za timu zote kuguswa. Taarifa zinazohusiana Kandanda , Michezo Pasi nzuri kutoka kwa Aron Ramsey iliyomkuta Theo Walcott ambaye bila kusita naye aliunganisha hadi kwa Kieran Gibbs aliyelitazama lango la Fenerbahce na kuandika bao la kwanza kwa Arsenal kunako dakika ya 51 ya mchezo. Dakika chache baadaye Arsenal waliendelea kulisakama lango la Fenerbahce, lakini Aron Ramsey aliongeza matumaini ya kutopoteza mchezo wa pili na kuwapa raha mashabiki wa Ashburton Grove kwa kufung...

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUHUSISHWA KATIKA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA'' SOMA HAPA

MSANII Wa Muziki wa Bongofleva mwenye jina kubwa Town na mwenye Mkwanja mkubwa hapa nchini Nasseeb Abdulmaliki “Diamond Platnumz” amejitokeza na kukanusha kuwa hahusiki na biashara ya madawa ya kulevya.   Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa za Diamond kujihusisha na biashara hiyo hasa kutokana na ukaribu wake na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini.  Taarifa zaidi zinasema ni wafanyabiashara hao waliohusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kifo chake ziligubikwa na matumizi ya madawa ya kulevya. Akikanusha taarifa hizo Diamond amesema  :   “ Ni kweli mimi nina pesa za kutosha kuniwezesha kuishi maisha ninayotaka lakini sijawahi kujihusisha na biashara hiyo . ... "Kufanya kazi kwa bidii kunalipa na kazi yangu inaonekana na ndiyo inayoniwezesha kuwa na fedha ambazo leo watu wameanza kuzitilia shaka. Sielewi nia ya watu haw...

Kenya yasaini Dola Bilioni 5 na China

Kenya imesaini mkataba na China ambao unatoa dola bilioni tano kuimarisha huduma za Reli,Kawi na Uhifadhi wa Wanyama Pori kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.Makubaliano hayo yaliafikiwa katika ziara ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini China. Hii ndio ziara ya kwanza ya Rais Kenyatta tangu kuchaguliwa hapo mwezi Machi mwaka huu.Serikali ya Kenya imepongeza mkataba huo na kusema utasaidia nchi kukua kiuchumi na kuboresha maisha ya raia wake. Mwenyeji wa Kenyatta, Rais wa ChinaXi Jinping , ameelezea kuridhishwa kwake na juhudi za serikali ya Bw Kenyatta katika kuimarisha taifa la Kenya. Uhusiano kati ya Uhuru Kenyatta na dola za magharibi umedorora kufuatia mashtaka dhidi yake katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita-ICC. Kenyatta anatarajiwa kwanza kesi dhidi yake baadaye mwaka huu. Ametuhumiwa kwa kufadhili ghasia za baada ya uchaguzi wa...

Mwanamke ajilipua kwa petroli baada ya mumuwe kuoa mke wa pili huko Geita.

MWANAMKE mmoja ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyankumbu, Kata ya Kalangalala mkoani  Geita amenusurika kifo baada ya kujimwagia mwilini mafuta ya petroli kisha kujilipua baada ya mumewe kuoa mke wa pili.   Imeelezwa kuwa mwanamke huyo, Anastazia Kubezya (28) Agosti 8 mwaka huu aliamua kujimiminia petroli mwili mzima kabla ya kuchukua kiberiti na kujilipua, hali iliyosababisha  akimbizwe katika Hospitali ya Geita alikolazwa katika wodi namba saba kwa matibabu. Akizungumza na mwandishi wetu, Consolata Raphael ambaye ni dada wa majeruhi huyo alidai kuwa chanzo cha mdogo wake huyo kufikia hatua ya kutaka kutumia njia hiyo ya mkato kwa lengo la kujiua ni wivu wa mapenzi. Consolata alisema: “Siku ya tukio shemeji yangu George Kubezya (mume wa majeruhi), alifika nyumbani kwa mdogo wangu wa kiume akidai kuwa mkewe huyo anatishia kujiua baada ya kuoa mke wa pili.   “Tukiwa tunaendelea kujadiliana mara alitokea mkewe Kubezya akiwa na viatu vya mwanaye...
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia kwa mahojiano Mbunge wa Nyamagana jijini humo,Mh Ezekiel Wenje kwa madai ya kuongoza maandamano yaliyosambaratishwa na polisihapo jana kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi

24 WAITWA TAIFA STARS KUIVAA GAMBIA

NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM. Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameita kambini wachezaji 24 kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo. Wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam. Makipa walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David Luhende (Yanga). Viungo Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Boko (Azam), Thomas Ulimweng...