Skip to main content

Posts

DOWNLOAD NAY WA MITEGO - LOWASSA - MP3.

CLIIP NYUMA YAPAZIA TV ONLINE 1

Yaliyojiri Jijini Tanga leo

 Pamoja na Wapeperusha Bedera za Vyama vyao kuwania Ubunge jimbo la tanga walivyorudisha fomu: Mbunge mtetezi na mwakilishi wa CCM mh.  Omari R Nundu  Alingia kimnya kimnya Ofisini kwa Mkurugenzi wa Jiji la Tanga kunako saa nne Asubuhi akisindikizwa na Wana CCM wapatao nane mpaka 10 hivi.   Pia Chama cha Wananchi CUF kiliingia kwa Vishindo kwa Msafara wa Magari na Honi wakimsindikiza Mpeperusha bendera wao Mh. Mussa Mbaruku, akina mama na baba wakiwa na vijana walionekana wakiwa na Hamasa katika kutimiza zoezi hilo la kurudisha Fomu. hii ilikuwa ni kama saasaba kasoro hiv

Tume ya Uchaguzi (NEC) imewaengua wagombea urais wa vyama vya Ada/Tadea, DP, CCK na AFP leo kwa maelezo kuwa wamekosa vigezo vya kugombea nafasi hiyo kubwa ya uongozi hapa nchini.

Kwa mantiki hiyo, Mchungaji Christopher Mtikila (DP), Godfrey Malissa (CCK) na John Chipaka (Ada-Tadea) hawatashiriki katika kinyang’anyiro hicho baada ya fomu zao kuonekana kuwa zina kasoro huku mgombea urais wa AFP, Omari Sombi akiungana na wanasiasa hao kutogombea baada ya kushindwa kurejesha fom u ya urais. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, wagombea wa vyama vinane kati ya 12 vilivyochukua fomu, wamekidhi matakwa ya sheria ya mchakato huo, hivyo wanaruhusiwa kuanza kampeni rasmi kesho. Amewataja wagombea waliopitishwa na NEC ni Dk. John Magufuli (CCM), Edward Lowassa (Chadema), Fahmi Dovutwa (UPDP), Macmillan Lyimo (TLP) na Chief Lutalosa Yemba (ADC). Wengine ni Anna Mghwira (ACT-Wazalendo) na Hashimu Rungwe (Chaumma) na Malik Kasambala (NRA). (C) Mwananchi Je, Tutarajie Mchungaji Christopher Mtikila Kutinga Mahakamani kupinga katazo hilo??

Salva Kiir akataa kutia sahihi mkataba

Salva Kiir Serikali ya Sudan Kusini imekataa kusaini mkataba uliotarajiwa kuleta amani na kumaliza mapigano yaliyodumu nchini humo kwa zaidi ya miezi ishirini. Hata hivyo waasi na makundi ya upinzani wamesaini kwa upande wao. Serikali imeomba kuongezewa siku kumi na tano zaidi kushauriana juu ya mapendekezo hayo. Waziri kutoka Uingereza anayesimamia maswala ya Afrika ameitaka serikali ya Sudan Kusini kutia sahihi mkataba huo haraka iwezekanavyo. Amesema kuwa watu hawafai kusheherekea hadi pale rais Kiir atakapotia sahih

Tchetche, 3-5-2 tishio kwa Yanga

Kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm amesema hana wasiwasi na mfumo wa 3-5-2 unaotumiwa na Azam FC tayari ameshapata mbinu ya kuwamaliza katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Jumamosi kwenye