Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2014

DULLAH WA MICHANO SASA KAZI MOJA.

WASANII WANAOUNDA KUNDI LA AKILI MUSIC TEAM WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA LEO,DULLA WA MICHANO,MORRIS,D.DOCTOR,VALENTAIN,KIDANI,MWANDEI, DAN TOUCH PRODUCER,JOJO,SMART BUSINESS NA TSETSEFLY. MSANII DULAH WA MICHANO WA TATU KUTOKA KUSHOTO AKIFURAHIA JAMBO NA WASANII WENZAKE MARA BAADA YA KUMALIZA KUREKODI WIMBO WAO MPYA LEO.

Breakng news Boti ya Kilimanjaro 2 yanusurika kuzama eneo la Nungwi

Habari zinasema kuwa boti ya Kilimanjaro 2 iliyokuwa ikitokea Pemba kuelekea Unguja imepigwa na dhoruba na kusurika kuzama katika eneo la nungwi.

Jenerali wa Sudan Kusini auwawa Bor.

Mmoja wa wanajeshi wa jeshi la Sudan Kusini. Mapigano makali yamezuka nje ya mji mkuu wa Sudan Kusini wa Bor na Jenerali mmoja wa jeshi la Sudan Kusini ameuwawa. Mwandishi wa BBC anasema vikosi vya serikali vinazidi kuelekea karibu na mji wa Bor ambapo kumekuwa na mapigano ya kutegeana baina ya majeshi ya serikali na vikosi vya waasi vinavyomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar. Mwandishi wetu amesema pia ameshuhudia miili ya watu ikiwa chini na vifaru vikiwa vimelipuliwa vibaya pembezoni mwa barabara. Pande pinzani nchini humo zinataraji kuanza mazungumzo ya ana kwa ana mjini Adis Ababa kujaribu kumaliza wiki tatu za mapigano. Kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Sudan kusini Nial Deng Nial amesema kuwa ni muhimu kwamba viongozi kuzungumzia kuhusu kusitishwa kwa vita.

Wasanii wanunua stika kwa pauni ya England

Dar es Salaam.  Tasnia ya sanaa imeendelea kuandamwa na changamoto nyingi ikiwamo wasanii kununua stika za kazi zao kwa pauni ya Uingereza badala ya shilingi ya Tanzania. Mfumo huo wa ununuaji wa stika zinazobandikwa katika makasha ya kazi zinazoandaliwa na wasanii hao hutolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ambayo imethibitisha jambo hilo, huku ikieleza kuwa wanauza kwa pauni kwa sababu mtengenezaji wa stika hizo akaunti yake ipo mwenye pauni, siyo shilingi. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wasambazaji wa kazi hizo, wasanii na uongozi wa sanaa nchini walisema tangu kuanza rasmi kwa mfumo huoJulai 2013, kumekuwa na hali ya sintofahamu kutokana na stika hizo kuwa adimu na zinapopatikana kuuziwa kwa fedha za nje kinyume na makubaliano ya serikali na wasanii juu ya mfumo huo. Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (Taff), Simon Mwakifamba alisema stika hizo kuuzwa kwa pauni ni changamoto mpya inayoukumba mfumo wa urasimishaji wa kazi za wasanii na kupoteza maana nzima ya z

BOBAN ARIPOTI COASTAL UNION TANGA.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam   KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Coastal Union yenye maskani jijini Tanga, Haruna Moshi ‘Boban’, ameripoti mkoani Tanga kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na mzunguuko wa pili wa ligi ya Tanzania Bara.     Haruna Moshi Boban pichani. Kuripoti kwa Boban kunashusha presha kutoka kwa wadau wa timu hiyo wanaosema kuwa kiungo huyo amekuwa mtovu wa nidhamu kwa kuchelewa kuripoti kambini.   Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa timu ya Coastal Union, Hafidh Kido, alisema kuwa Boban aliafiki kujiunga na wenzake mapema wiki hii ili kuendelea na mazoezi ya pamoja.   Alisema kuwa kujiunga na wenzake katika maandalizi ya michuano ya Vodacom ni sehemu ya kujiweka sawa zaidi.   “Baada ya kumaliza ratiba yake kama alivyotoa taarifa kwa viongozi wake, Boban amejiunga na wenzake.   “Tunaamini mambo yatakuwa mazuri kwa kiungo huyo ambaye uwezo wake hapana shaka unajulikana na kuheshimika sana,” alisema.   Boban ni miong

Boban ni mchezaji halali wa CUSC

 Kikosi cha maangamizi cha CUSC....  Hiki ni kipande cha gazeti la leo Jumatano Januari 1,2014 gazeti Mtanzania kuhusu habari za Boban. Haruna Moshi, akimiliki mpira katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati akiitumikia CUSC kwenye mechi yake ya kwanza ligi kuu na Wagosi wa Kaya. Ilikuwa ni mechi dhidi ya Oljoro JKT, ambapo CUSC iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.   Ndugu zangu, WIKI hii kumekuwa na habari za upotoshaji juu ya kutimuliwa kwa kiungo mshambuliaji wa Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’, Haruna Moshi ‘Boban’. Ninaziita habari za upotoshaji kwasababu hazina ukweli, na mara nyingine mtu anaweza kuenda mbali zaidi na kufikiri kuwa kuna hujuma zinafanyika dhidi ya timu yetu ili wachezaji wasicheze kwa moyo wakati wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara, unaotarajiwa kuanza Januari 25 mwaka huu. Gazeti moja la michezo, jina tunalihifadhi limeripoti likimnukuu kiongozi mmoja wa Wagosi wa Kaya, jina pia tunalihifadhi kutokana na heshima yake; kuwa Co

Breaking news: Waziri wa fedha William Mgimwa afariki dunia