John Dilinga, 'DJ JD', nae akiwaeleza wanahabari jinsi alivyotapeliwa na Chameleone mwaka 2005. DJ mkongwe nchini, John Dilinga Matlou ‘DJ JD’, leo nae ameweka wazi utapeli aliowahi kufanyiwa miaka saba iliyopita na mwanamuziki raia wa Uganda, mwenye hulka ya utapeli, Joseph Mayanja Chameleone. JD, amewaeleza waandishi wa habari leo, waliokusanyika kwenye Hoteli ya The Atriums kwamba Chameleone siyo mtu mzuri anapokubaliana na mapromota, kwani hata yeye aliwahi kumtapeli dola za kimarekani 3,000, mwaka 2005. Alisema mbele ya waandishi wa habari: “Niliwasiliana na Chameleone moja kwa moja, akanikubalia kwenye tamasha langu lililokuwa linaitwa Wakilisha. Nilimlipa dola 3,000, baada ya kupokea fedha, hakuonekana tena na hata simu yangu akawa hapokei. “Aliendelea kunikimbia hivyo. Tatizo kubwa lipo kwa mapromota wa Kitanzania, hatuna ushirikiano kabisa. Kila alipokuja nchini kufanya shoo, nilimfuata promota husika lakini promota mwenyew