Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2012

ROMA AAMUA KUUZA WIMBO WAKE MPYA KWA SH. 3000 HUKU NIKKI WA PILI NAYE AKITUMIA M-PESA KUIUZA DVD YAKE

                                   Wasanii wanazidi kuwaza kila siku jinsi ya kukwepa kuibiwa kazi zao ambazo ni jasho lao wanalotoa booth baada ya kusumbua akili zao na kufanyia kazi vyema mtaji wa kipaji walichopewa na Mungu. Asilimia 90 ya wasanii wa Hip Hop hawapeleki kazi zao kwa wasambazaji bali huuza wenyewe ili kukwepa kuwafaidisha watu wengine kwa jasho lao. Staili ya uuzaji iliyopewa jina la ‘kuuuza tapes kwenye bag’ inazidi kupatiwa mbadala kama sio kuboreshwa ili kuwafikia watu wengi zaidi. Roma mkatoliki ambae ametambulisha wimbo wake alioupa jina la ‘2030’, wimbo ambao unasubiriwa kwa huwa hadi sasa na fans wake kibao waweze kuupakua kwenye mtandao, sasa amekuja na staili tofauti ambapo anauuza wimbo huo kwa Tsh. 3000 tu . Roma kupitia ukurasa wake wa facebook, ameelezea kuwa mteja wake atatuma pesa hiyo kwa njia ya simu pesa na email yake ama atatumiwa kwa njia ya Whasapp, kisha Roma atamtumia wimbo huo, lakini kwa ma

ASKARI ALIYEPIGA PICHA NA LEMA ATOROKA JESHINI

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema askari anayedaiwa kuwa jeshi hilo aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ametoroka. Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema jana kwamba pamoja na hatua yake ya kutoroka, jeshi litaendelea kumsaka kwa udi na uvumba ili kumhoji na kujiridhisha kama kweli ni mwanajeshi wake kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kifungu cha 147 cha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977. “Huyu kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini wakati tunaendelea na uchunguzi alitoroka katika nyumba aliyokuwa amepanga bila ya taarifa kwa baba mwenye nyumba,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza: “Askari huyo alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga mita chache karibu na Kituo cha Polisi cha Simanjiro, Arusha na alikuwa akijishirikisha na ulinzi shirikishi.” Alipoulizwa jina la askari huyo, Kanali Mgawe alijibu: “Yeye alikuwa anafahamika mtaani hapo kwa jina la kamanda.”

NI MR BLUU A . K . A KABAYSA LEO KATIKA MKESHA WA MWAKA MPYA NDANI YA JIJI LA MWANZA

Usiku wa leo yong bab lon  r Bluu atakinukisha ndani ya jiji la Mwanza katika usiku wa mwaka mpya aliyasema hayo katika radio kiss fm akifanya mahojiano leo mchana mr bluu amesemakuwa leo atawafuraisha mashabiki wake kwa kupitia nyimbo zake za kipindi na za sasa .Pia amewaambia mashabik wakae mkao wa kula kwa kusubiri tunzo  bomba za mwaka 2013.

Ndege ya Tanapa yaanguka, yajeruhi rubani

  NDEGE ndogo ya abiria mali ya Hifadhi ya Taifa ya Tanapa  yenye uwezo wa kubeba  watu  wanne aina ya C 182, imeanguka katika  eneo la Kasimba  umbali wa kilometa moja  kutoka katika  Uwanja wa Ndege wa Mpanda  uliopo katika Mkoa wa Katavi  na kumjeruhi rubani wa ndege hiyo. Akizungumza na vyombo vya habari, Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, Maulid  Mohamed alisema ajali  hiyo  ilitokea jana  majira saa 10 .55 jioni  katika   eneo la Kasimba lililopo ndani ya Kijiji  cha Nsemlwa   wilayani hapo. Mohamed aliitaja ndege hiyo iliyoanguka na kusababisha majeraha kwa rubani aliyetajwa kwa jina la Adam Athuman Kajwaa kuwa  ni aina ya C182. Mohamed  alieleza kuwa  ndege  hiyo   ilikuwa imetoka  katika uwanja wa ndege wa Mpanda ikielekea  katika Hifadhi ya Wanyamapori  ya Katavi.    Hata hiyo alisema kuwa ajali hiyo  ilitokea   umbali wa 

Kigogo NCCR-Mageuzi ahamia Chadema

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Lawrence Tara, amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet, wilayani Babati,  Mkoa wa Manyara tangu mwaka 2000, alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kupokewa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Godbless Lema. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kiongozi mwingine wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Ally Bananga. Tara alitoa sababu mbili zilizomfanya aihame NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema; upendeleo na dhuluma kwa watumishi wa chama hicho. Alidai kwamba baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa kigezo cha urafiki kama kifanyavyo chama tawala, CCM. Alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo mbovu ndani ya NCCR- Mageuzi, baada ya ch

Aunty Ezekiel Akiri Kufurahia Maisha ya Ndoa Japo Ndio Anaanza

MSANII mahiri wa filamu ambaye kwa sasa ni mke wa mtu Aunty Ezekiel , amerudi hivi karibuni kutoka Dubai wanakoishi na mume wake ameuambia mtandao wa DarTalk , kuwa maisha ya ndoa kwa upande wake yako safi kwani ndiyo kwanza anaanza hivyo hajajua machungu yake wala matatizo yake. Alisema kuwa anaamini kutokana na upendo wa dhati alionao kwa mume wake ndoa yake itakuwa yenye furaha siku zote kama ilivyo sasa kwani wanapendana kupita maelezo. “Kwa kweli nikisema sasa nitakuwa muongo kwani ndiyo kwanza nimeingia na unajua kwamba sina uzoefu wowote katika ndoa, lakini kwa muda huu nimekuwa naona yako pouwa kwa sababu upendo haujapungua ndiyo kwanza unaongezeka,” alisema. Hata hivyo kwa upande wa filamu alisema kuwa hajarudi kwa ajili ya kufanya kazi hiyo kwani kwa mwaka huu ndo amefunga ukurasa na hapo mwakani Mungu akijalia atafanya mchakato wa kurudi upya.

HAWA NDIOWAKALI WATAKAOLIWASHA MOTO JIJI LATANGA KESHO

  Hammer Q   Mkongwe Ruwa                                                                                               Brider Khan   Tng Squad Hammer Q Mfalme Wa Taarabu na Mduara Tanzania Kuuwakilisha" Usiku Wa Bata La Pwani  J.2 Hii Ndani Ya Tanga Club La Grand Lakasa Chika Akiwa Na H-Mbizo A.k.a Mkubwa Sn Pa1 Na T.n.g Squad,Mwanashost Mayna,Brider Khan Mzee wa Chuchuchu Aliyekua Mshindi wa Super Nyota Tanga 2912 Na..pamoja na raisi wa warembo Mkongwe Na Kuhakikisha Kila Kitu Kinakua Poa Kwenye Usiku Wa Bata La Pwani Na Mpango Mzima Utakua Ni Kwa kiingilo kidogo tu ch Buku 3000 Kwa Ladies & Babaz...Karibuni

HUSSEIN MACHOZI NA CPWAA NDANI YA NGOMA MPYA YA " READY TO GO".....

Katika mlolongo wa kazi za wasanii za funga mwaka ambapo kila msanii anafanya kila awezalo ili kutoa wimbo mpya, muunganiko Hussein Machozi pamoja na mkali wa Mission 12 O’clock, Cpwaa unaingia katika orodha hiyo. Kutokana na fununu tulizopata ni kwamba wawili hao wamekwisha kamilisha kupika ngoma kali iitwayo “Ready To Go”. Kazi hiyo imepikwa na producer Jayyson katika studio za Hip Palace Records kutoka kipande cha K’Nyama Dar es Salaam.Hussein Machozi amempa shavu CP kutokana na touch zake adimu na ambazo Hussein baada ya kufikiri sana aliona ndio zinafit kwa kazi hiyo. “Ready To Go” inakaribia kudondoka kwenye vyombo vya habari ndani ya muda usiopungua wiki moja sasa na matayarisho yake yanatoa kila sababu ya kuamini kuwa itakuwa ni Hit. Zawadi nyingine ya Krismasi kutoka kwaa Machozi.

KESHO BLOG HII INATIMIZA MWAKA MMOJA TOKEA KUANZISHWA SASA WEWE KAMA MDAU TUCHANE CHOCHOTE KISICHOKUFURAISHA NA KIPI KILIKUFURAISHA NDANI YA MWAKA MZIMA YA UWEPO WA BLOG HII ????????

DEC,/6/2011 TO DEC,/6/2012 HAPPY BIRTHDAY! MTOTO DAILY!

"Rushwa yazorotesha uchumi duniani"

                                           Waziri Mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras   Kwa mara nyingine, Dernmark, Finland na New Zealand zimekuwa na rikodi nzuri kwa mujibu wa Transparency International wakati Afghanstan, Korea Kasikazini na Somalia zikisalia mkiani katika kadhia ya rushwa. Kwa kuzingitia kipimo kinachoanisha sifuri - kama kiwango kibaya zaidi cha rushwa - mpaka 100 - ikiwa ndiyo rikodi nzuri kabisa, Dernmark, Finland na New Zealand zimefungana kwa kupata alama 90. Lakini Afghanstan, Korea Kaskazini na Somalia kila moja imepata alama 8. Hali ilivyo katika mataifa ya Kiarabu Pamoja na hayo, ripoti hiyo imeonesha kumekuwa na mafanikio kidogo sana katika mataifa ya Kiarabu yaliyokumbwa na vuguvugu la kisiasa. Mataifa hayo ni pamoja na Misri na maeneo mengine ya Mashariki ya Kati. Mataifa ambayo ni kiini cha mgogoro wa madeni yameendelea kupata alama duni zaidi, ambapo tatizo hilo la mgogoro wa madeni limeonekana kama chachu ya vitendo vya rushwa. U