HATIMAYE msaani maarufu wa vichekesho nchini, Gilliady Severine a.k.a Masai Nyotambofu, ametoa siri yake ya kutumia lafudhi ya jamii ya Kimasai katika kazi yake ya sanaa ya maigizo na vichekesho. Akizungumza na blog hii jijini hapa juzi, Nyotambofu alisema kuwa, yeye aliamua kutumia lafudhi ya Kimasai baada ya kubaini kuwa ni ngumu na hata waliyokuwa wakijaribu kuitumia katika sanaa mbalimbali, hawakuweza kukidhi mahitaji ya lafudhi ya lugha hiyo. Msanii huyo amekuwa akisikika katika matangazo mbalimbali yanayorushwa na vituo vya radio hapa nchini, hasa ya uhmasishaji wa kuacha pombe, yaani ‘ulevi noma’ lilitolewa na Idara ya Ustawi wa Jamii wakishirikiana na Jeshi la Polisi. “Ndugu mwandishi, niliamua kutumia lafudhi ya Kimasai, kwani nilishafanya utafiti na kubani kuwa, lugha hii ni ngumu kuiga, pia niliangalia wasanii ambao walikwisha kujaribu kuitumikia lafudhi ya Kimasai, nikaona hawajakidhi kabisa ndipo nikaamuua kuitumia na mpaka sasa najivunia nimeweza,” alis