Skip to main content

Posts

PICHA 10 ZA TANGA ALL STAR WAKATI WAKUFANYA WIMBO WAKUMUENZI SHARO MILIONEA.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva kutoka Tanga walikutana Tongwe Records Masaki ilikufanya wimbo kwa ajili ya Marehemu Sharo Milionea. Dani Msimamo ,Cpwaa na Roma Dani Msimamo , Roma,Mapacha TNG na R ose N dauka Q Chief Aki andika mis tari ya Chorus y a wimbo huo. Mr Misosi , Q Chief na TNG TNG ,Dani M simamo , Kassim Mganga ,Cpwaa. J Murder na L Single J Murder ,Roma wakiskiliza wimbo wa Ta nga All Stars .

HAPPY BIRTHDAY! Upendo Mushi

  Happy birthday! Mtoto mlito m-mungu akupe maisha marefu    Namshukuru mwenyezi mungu kwa kuendelea kunibariki,kunijalia afya njema,amani na upendo mpaka leo hii si kama ni mwema sana bali ni kwa neema yake mwenyezi mungu isiyo na kikomo.nawashukuruni wote ndugu zangu kwa kunitakia maisha mema yenye amani na baraka zake mwenyezi mungu!nami niwatakie maisha mema na tupendane kwani 2 watoto wa baba mmoja.!!!!!!!

BURIANI SHARO MILIONEA!!!!!!!!!!!!!!!!

Gari alilokuwa akiendesha Sharomilionea linavyoonekana katika eneo la ajali. Baadhi ya wananchi wakilitazama gari alilokuwa akiendesha Sharomilionea na kuharibika vibaya baada ya kupinduka na kumsababaishia umauti. Wananachi wakiendelea kutazama mabaki ya gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiliendesha Sharomilionea kabla halijapinduka na kumsababaishia umauti. (Picha zote: Kwa hisani ya blog ya Libeneke la Kaskazini)  . Hapa linavyoonekana gari alilokuwa akiendesha marehemu Sharomilionea linavyoonekana kwa nyuma. Mbunge wa Jimbo la Muheza, Herbet Mtangi (kushoto) akiwa katika Hospitali Teule ya Muheza ulikohifadhiwa mwili wa marehmu Sharomilionea. Hatuamini... tunataka kuhakikisha! Baadhi ya wananchi wakiwa nje ya chumba cha maiti cha Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza kushuhudia mwili wa marehemu Sharomilionea aliyefariki kwa ajali ya gari.  Mbunge wa Jimbo la Muheza, Herbet Mta...

R.I.P SHARO MILIONEA!!!!!!!!!!!!!!!

Watu waliamini ukitaka kumchekesha mtu lazima utumie nguvu,uweke matambaa tumboni,uvae nguo za ajabuajabu....Ila mimi niliamua kuwa tofauti zaidi niliamua kuwachekesha watu kisafi,bila kutumia nguvu bali kuwa mbunifu zaidi'' ~SHARO MILIONEA Ni kweli ulileta mabadiliko kwenye sekta ya uchekeshaji na ulikubalika na rika lote Pumzika Kwa Amani Mwana tanga,mtanzania mwenzetu SHARO BARO SHARO MILIONEA r.i.p

YANAYOJIRI KWENYE MSIBA WA SHARO MILLIONEA:

Hali ya mzee King Majuto presha imepanda na hali kuzidi kuwa mbaya kutokana na kupata taarifa za msiba wa Sharo Milionea. Mjomba wa marehemu Sharo Millionea, Bwana Omary Fundikira asema marehem u anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho, Jumatano. Hii ni kutokana na msanii mwenzake John Maganga kuzikwa leo. Mkuu wa polisi mkoa wa Tanga RPC Costantine Massawe asema Hussein Ramadhani (Sharo Milionea) alikuwa mwenyewe katika gari na ilipotokea ajali gari lilimrusha nje na kufariki hapohapo. Pia rafiki wa marehemu bwana Mohamed Ismail ambaye ndiye aliyemuazimisha gari alilopata nalo ajali, asema ilitakiwa waongozane kwenda Tanga pamoja ila alishindwa maana alipata majukumu mengine.

HIKI NDO CHANZO CHA AJALI YA SHARO MILIONEA PAMOJA NA SIKU KAMILI YA MAZISHI

 Habari za uhakika kuhusiana na chanzo cha kifo cha msanii Hussein Ramadhan a.k.an Sharo milionea ni kwamba gari yake aina ya Toyota harrier ilipata pancha tairi la upande wa kulia na kukosa mwelekeo kisha ikaacha njia na kuelekea mtaroni lakini ule mtalo haukuizuru sana gari hiyo ikaruka na kuingia katika shamba la maindi.  Kitu kilichoshangaza wengi ni sehemu ambayo si hatarishi sana kiudereva sababu iko tambarare na kona si kali eneo hilo.    Chanzo cha habari kinaendelea kufafanua kuwa baada ya gari kuacha njia ilienda kugonga mti mkubwa na kuung'oa baada ya kuuchana katikati kutokana na gari ilivyokuwa mwendo kasi. Mwili wa marehemu ulitupwa nje ya gari baada ya kugonga mti huo ambapo gari hiyo iliharibika vibaya kuanzia kwenye roof hadi vioo vyote kupasuka japo vizuizi vilifunguka lakinini havikusaidia.  Kishindo kikubwa cha mlio wa pancha kilisikika kwa wakazi wa kijiji hiko na kuamua kujitokeza kujua nini kimejili pale na wakati wa...

KIFO CHA MSANII SHARO MILIONEA RIPOTI KAMILI HII HAPA..PICHA YA MWILI WAKE

Jana majira ya saa mbili usiku, msanii na mchekeshaji maarufu nchini Sharo Milionea amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari wakati akitoa Dar es Salaam kueleka wilayani Muheza, Tanga. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe Hussein Ramadhani au Sharo Milionea alikuwa akiendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier. Alipofika maeneo ya maguzoni njekidogo na wilayani MUHEZA gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa, likagonga mti na kusababisha kifo chake na yeye kutokea mbele ya kioo cha gari na kutupwa mbali. Alisema Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza. Aliongeza kuwa hakuna kona kali wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali. Gari lake imehifadhiwa mahali salama kwakuwa limeharibika vibaya na kwamba kwenye gari alikuwa mwenyewe. Habari kuhusu kifo chake zilianza kuenea jana usiku ambapo kwa upande wa rafiki yake wa karibu Kitale amesema alikuwa akiipiga simu ya Sharo Milionea iliyokuwa iki...