kassim Mganga Kwa ufupi Ukimuona kwa mbali unaweza ukahisi kuwa ni kiumbe mzito, lakini ukimpa muda wa kurembesha jukwaa lako kwa burudani, utagundua kuwa umbo lake na sanaa anayofanya ni vitu viwili tofauti. By Henry Mdimu Ukiwa msikilizaji mzuri wa muziki, hasa wa kizazi kipya kuna wakati utakubaliana na kauli isemayo katika nyimbo bora zilizotoka mwaka huu ambazo zina mafunzo ambayo mabinti hupenda kuyasikia, hutaacha wimbo uitwao “Subira” wa kijana mdogo kutoka Tanga, Kassim Hemed Mganga. Ukimuona kwa mbali unaweza ukahisi kuwa ni kiumbe mzito, lakini ukimpa muda wa kurembesha jukwaa lako kwa burudani, utagundua kuwa umbo lake na sanaa anayofanya ni vitu viwili tofauti. Ana uwezo wa kusherehesha kwa takriban masaa matano bila kuchosha mashabiki wake. Kibao chake cha “Subira” ndiyo habari ya mjini; kwenye pub, baa, klabu, bodaboda, bajaj, redioni na simu za mikononi ni “Subira, Subira Subira”. Ni kibao kilicho katika miondoko ya pwani, hasa chakacha, n