Hussein Semdoe, Tanga KUMBE mapango maarufu ya Amboni yaliyopo katika Kata ya Kiomoni, Tarafa ya Chumbageni wilayani Tanga, Mkoa wa Tanga, ni sehumu muhimu ya kujivunia na ya kihistoria ya nchi yetu, kutokana na miamba ya mapango hayo kituo cha hija kwa watu mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania . Kutokana na umuhimu wa mapango hayo watu 42, wamekuwa wakitembelea kila siku kwa ajili ya kufanya matambiko na kutoa sadaka kwa kizimu. Mambo yanayovutia Mapango ya Amboni Mambo manne yanayowavutia wataliii katika mapango hayo ni: mawe yakua kama mimea, sanamu ya Bikira Maria, maandiko ya Quran takatifu, miamba inayofanana na kochi na meli, na barabara zinazopita ndani ya mapango hayo. Kwa mujibu wa utafiti, miamba hiyo inakua kwa kasi zaidi katika kipindi cha mvua, ukilinganisha na msimu wa kiangazi. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ukuaji wa miamba hiyo ulikuwa kwa milimeta 0.5 na iliwahi kuongezeka kwa kasi ya milimeta saba katika kila baada ya miaka 100.