Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2012

PICHA 10 ZA TANGA ALL STAR WAKATI WAKUFANYA WIMBO WAKUMUENZI SHARO MILIONEA.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva kutoka Tanga walikutana Tongwe Records Masaki ilikufanya wimbo kwa ajili ya Marehemu Sharo Milionea. Dani Msimamo ,Cpwaa na Roma Dani Msimamo , Roma,Mapacha TNG na R ose N dauka Q Chief Aki andika mis tari ya Chorus y a wimbo huo. Mr Misosi , Q Chief na TNG TNG ,Dani M simamo , Kassim Mganga ,Cpwaa. J Murder na L Single J Murder ,Roma wakiskiliza wimbo wa Ta nga All Stars .

HAPPY BIRTHDAY! Upendo Mushi

  Happy birthday! Mtoto mlito m-mungu akupe maisha marefu    Namshukuru mwenyezi mungu kwa kuendelea kunibariki,kunijalia afya njema,amani na upendo mpaka leo hii si kama ni mwema sana bali ni kwa neema yake mwenyezi mungu isiyo na kikomo.nawashukuruni wote ndugu zangu kwa kunitakia maisha mema yenye amani na baraka zake mwenyezi mungu!nami niwatakie maisha mema na tupendane kwani 2 watoto wa baba mmoja.!!!!!!!

BURIANI SHARO MILIONEA!!!!!!!!!!!!!!!!

Gari alilokuwa akiendesha Sharomilionea linavyoonekana katika eneo la ajali. Baadhi ya wananchi wakilitazama gari alilokuwa akiendesha Sharomilionea na kuharibika vibaya baada ya kupinduka na kumsababaishia umauti. Wananachi wakiendelea kutazama mabaki ya gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiliendesha Sharomilionea kabla halijapinduka na kumsababaishia umauti. (Picha zote: Kwa hisani ya blog ya Libeneke la Kaskazini)  . Hapa linavyoonekana gari alilokuwa akiendesha marehemu Sharomilionea linavyoonekana kwa nyuma. Mbunge wa Jimbo la Muheza, Herbet Mtangi (kushoto) akiwa katika Hospitali Teule ya Muheza ulikohifadhiwa mwili wa marehmu Sharomilionea. Hatuamini... tunataka kuhakikisha! Baadhi ya wananchi wakiwa nje ya chumba cha maiti cha Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza kushuhudia mwili wa marehemu Sharomilionea aliyefariki kwa ajali ya gari.  Mbunge wa Jimbo la Muheza, Herbet Mtangi ni m

R.I.P SHARO MILIONEA!!!!!!!!!!!!!!!

Watu waliamini ukitaka kumchekesha mtu lazima utumie nguvu,uweke matambaa tumboni,uvae nguo za ajabuajabu....Ila mimi niliamua kuwa tofauti zaidi niliamua kuwachekesha watu kisafi,bila kutumia nguvu bali kuwa mbunifu zaidi'' ~SHARO MILIONEA Ni kweli ulileta mabadiliko kwenye sekta ya uchekeshaji na ulikubalika na rika lote Pumzika Kwa Amani Mwana tanga,mtanzania mwenzetu SHARO BARO SHARO MILIONEA r.i.p

YANAYOJIRI KWENYE MSIBA WA SHARO MILLIONEA:

Hali ya mzee King Majuto presha imepanda na hali kuzidi kuwa mbaya kutokana na kupata taarifa za msiba wa Sharo Milionea. Mjomba wa marehemu Sharo Millionea, Bwana Omary Fundikira asema marehem u anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho, Jumatano. Hii ni kutokana na msanii mwenzake John Maganga kuzikwa leo. Mkuu wa polisi mkoa wa Tanga RPC Costantine Massawe asema Hussein Ramadhani (Sharo Milionea) alikuwa mwenyewe katika gari na ilipotokea ajali gari lilimrusha nje na kufariki hapohapo. Pia rafiki wa marehemu bwana Mohamed Ismail ambaye ndiye aliyemuazimisha gari alilopata nalo ajali, asema ilitakiwa waongozane kwenda Tanga pamoja ila alishindwa maana alipata majukumu mengine.

HIKI NDO CHANZO CHA AJALI YA SHARO MILIONEA PAMOJA NA SIKU KAMILI YA MAZISHI

 Habari za uhakika kuhusiana na chanzo cha kifo cha msanii Hussein Ramadhan a.k.an Sharo milionea ni kwamba gari yake aina ya Toyota harrier ilipata pancha tairi la upande wa kulia na kukosa mwelekeo kisha ikaacha njia na kuelekea mtaroni lakini ule mtalo haukuizuru sana gari hiyo ikaruka na kuingia katika shamba la maindi.  Kitu kilichoshangaza wengi ni sehemu ambayo si hatarishi sana kiudereva sababu iko tambarare na kona si kali eneo hilo.    Chanzo cha habari kinaendelea kufafanua kuwa baada ya gari kuacha njia ilienda kugonga mti mkubwa na kuung'oa baada ya kuuchana katikati kutokana na gari ilivyokuwa mwendo kasi. Mwili wa marehemu ulitupwa nje ya gari baada ya kugonga mti huo ambapo gari hiyo iliharibika vibaya kuanzia kwenye roof hadi vioo vyote kupasuka japo vizuizi vilifunguka lakinini havikusaidia.  Kishindo kikubwa cha mlio wa pancha kilisikika kwa wakazi wa kijiji hiko na kuamua kujitokeza kujua nini kimejili pale na wakati wanafika hapakuwa na

KIFO CHA MSANII SHARO MILIONEA RIPOTI KAMILI HII HAPA..PICHA YA MWILI WAKE

Jana majira ya saa mbili usiku, msanii na mchekeshaji maarufu nchini Sharo Milionea amefariki dunia kwa ajali mbaya ya gari wakati akitoa Dar es Salaam kueleka wilayani Muheza, Tanga. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe Hussein Ramadhani au Sharo Milionea alikuwa akiendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier. Alipofika maeneo ya maguzoni njekidogo na wilayani MUHEZA gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa, likagonga mti na kusababisha kifo chake na yeye kutokea mbele ya kioo cha gari na kutupwa mbali. Alisema Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza. Aliongeza kuwa hakuna kona kali wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali. Gari lake imehifadhiwa mahali salama kwakuwa limeharibika vibaya na kwamba kwenye gari alikuwa mwenyewe. Habari kuhusu kifo chake zilianza kuenea jana usiku ambapo kwa upande wa rafiki yake wa karibu Kitale amesema alikuwa akiipiga simu ya Sharo Milionea iliyokuwa iki

Waasi wa M23 wakutana na Kabila

                                                          Waasi wa M23 wametangaza   kuanzisha mazungumzo na rais wa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo Joseph Kabila,saa chache baada ya mkutano wa kimkoa kulitaka kundi hilo kusitisha mashambulizi yake mashariki mwa nchi hiyo. Wakipata ushindi mdogo kwa viongozi hao wa kimkoa, kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo la waasi wa mashariki ya jamhuri ya Congo Jean -Marie Runiga Lugerero , amesema kuwa alikuwa na mazungumzo ya awali na Kabila baada ya mkutano huo uliofanyika mjini Kampala kumalizika. Wakati hakualikwa binafsi katika mkutano huo , Runiga Lugerero aliliambia shirika la habari la AFP kuwa alifanikiwa kukutana na Kabila kwa kupitia upatanishi wa rais wa Uganda Yoweri Museveni, ambae alitarajiwa kufanya nae mazungumzo hii leo Jumapili(25.11.2012).   Viongozi wa Afrika wakikutanamjini    Kampala, rais Kabila (kulia) na Museveni (katikati) "Hali ilikuwa tete lakini baadaye , kila upande ulipunguza

Rais Morsi aahidi demokrasia

Rais Mohamed Morsi amesisitiza Ijumaa (22.11.2012)kuwa Misri inaelekea katika "uhuru na demokrasia",baada ya kujilimbikizia madaraka makubwa,hali ambayo imezusha mapambano kati ya wale wanaomuunga mkono na mahasimu. "Uthabiti wa kisiasa, uthabiti wa kijamii na uthabiti wa kiuchumi ndio kitu ninachokitaka na ndio ninachokifanyia kazi," ameuambia mkusanyiko wa wafuasi wake nje ya Ikulu ya nchi hiyo. Wapinzani wa Morsi walianza hatua ya kukalia eneo la Tahrir kwa muda wa wiki moja, eneo ambalo linatambulika kuwa ishara ya maandamano ambayo yameuangusha utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak mwaka jana, na wametoa wito wa maandamano makubwa zaidi siku ya Jumanne.   Waandamanaji wakivamia ofisi ya chama cha udugu wa Kiislamu na kuchoma moto mali mbali mbali Magari yachomwa moto Mapambano yalizuka kati ya polisi na waandamanaji karibu na uwanja huo, huku waandamanaji wakichoma moto gari la polisi, wamesema watu walioshuh

Zitto afichua siri yake na JK

Rais Kikwete na Zitto Kabwe   MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amefichua siri ya uhusiano wake na Rais Jakaya Kikwete kuwa, unatokana na kuheshimu mchango wake anaoutoa kwa taifa. Kutokana heshima hiyo, Zitto anasema ndiyo maana Rais Kikwete hakufika jimboni kwake katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 na mwaka 2010 kumnadi mgombe wa CCM. Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema hayo katika mahojiano maalum na Mtandao wa Jamii Forum juzi. Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, jana alilithibitishia gazeti hili kwamba alihojiwa na mtandao huo kwa saa nane. “Kweli ni mahojiano baina yangu na Jamii Forum. Kwa Kfupi ni kwamba, yalikuwa  mahojiano ya saa nane, kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa kumi jioni na walionihoji kwa njia ya mtandao walikuwa wakituma maswali na mimi nawajibu,” alisema Zitto. Alisema yeye na Rais Kikwete wana uhusiano nje ya siasa na hata siku moja hawajadili mambo ya vyama vy

Kikosi cha Coastal Union kinachoanza dhidi ya.Young Africas leo

Kikosi kinachoanza Leo na Yanga ni hiki hapa....   1.Juma Mpongo 2.Ismail Suma 3.Juma Jabu 4.Jamal Macherenga 5.Kibacha 6.Jerry 7.Soud Mohamed 8.Razak 9.Daniel Lyanga 10.Atupele Green 11.Suleiman Selembe Reserve 1.Chove 2.Hamis Shengo 3.Said sued 4.Abdy Banda 5.Othmani Mani 6.Lameck Dyton 7.Aziz Gilla Team Coach-Hemed Morroco

KUTAMBIANA KWA WASHABIKI WA COAST UNION NA YANGA

ONA JINSI MASHABIKI WA COASTAL UNION NA YANGA WANAVYOCHIMBIANA MKWARA JIJINI TANGA LEO... WAKATIZA MITAANI JIJINI TANGA KWA TAMBO NA VIJEMBE ... VIINGILIO MECHI YAO KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI VYAANDIKA REKODI... WATU WAANZA KUFURIKA UWANJANI KUANZIA SAA 7:00 MCHANA....! Yanga leo hawatoki...! Shabiki maarufu wa klabu ya Coastal Union, Ibrahim 'Ibra' akionekana katika Barabara ya 8 jijini Tanga mchana huu baada ya kukamilisha michoro yake mwilini akiwachiomba mkwara Yanga kabla ya kwenda uwanjani kuishangilia timu yake itakayocheza jioni ya leo dhidi ya Yanga kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo Novemba 11, 2012.  Chezea Coastal wewe...! Shabiki Ibra wa Coastal akionyesha mchoro wake kwa mbele kuipiga mkwara Yanga kabla ya mechi yao ya leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Hapa ni katika Barabara ya 8 jijini Tanga mchana huu Novemba 11, 2012. Mashabiki wa Yanga wakiandamana

Wafungwa wawatoa kwa nguvu FFU kwenye nyumba

BAADHI ya wafungwa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wanadaiwa kutumiwa na kigogo mmoja wa Polisi kuwatoa kwa nguvu askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kwenye nyumba walizokuwa wakiishi katika Kambi Kuu ya mjini Moshi. Tofauti na ilivyozoeleka ambapo hushuhudiwa FFU wakitumika kusambaratisha mikusanyiko ya watu wenye lengo la kuhatarisha amani, askari hao walitolewa kwa nguvu kwenye nyumba hizo na wafungwa hao ambao wanadaiwa kutoa vyombo vyao nje. Tukio hilo lililowaacha vinywa wazi watu wengi mkoani Kilimanjaro, limewapata FFU waliokuwa wakiishi kwenye nyumba tatu zilizopo katika kambi kuu ya polisi mjini Moshi. Taarifa zinadai FFU hao ilibainika kuwa   hawakupaswa kuishi katika nyumba hizo, badala yake polisi wa kawaida ndio waliopaswa kuishi, hivyo waliondolewa ili polisi hao waingie. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alipoulizwa na gazeti hili alikiri kutokea kwa tukio hilo, lakini akasema: “Hayo ni masuala ya ndani ya polisi, siyo ya kuyaandika

Chama cha makahaba chasajiliwa rasmi

Rais wa Malawi,Joyce Banda   Kwa ufupi  Muda wa kujadili kwa pamoja matatizo yanayowakabili ndio huu. Mnajua namna Polisi na Mahakama vinavyowabana na kwamba mnahitaji kupata huduma nzuri za kulinda afya zenu na afya ya uzazi bila kipingamizi,” alisema mwanasheria wa haki za binadamu, Chrispin Sibande alipokuwa akizungumza na kundi la wateja wake wapatao 50 ambao ni makahaba.  ZAIDI ya makahaba 2000 nchini Malawi wameungana kwa ajili ya kupinga manyanyaso wanayoyapata na kuboresha mazingira ya afya, baada ya kuzindua rasmi chama cha kuwatetea juzi. Kundi hilo linaundwa na vyama visivyo vya kiserikali vya ndani na nje ya nchi hiyo, ikiwa ni la kwanza kutambuliwa rasmi na kupewa usajili katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambapo biashara ya ukahaba inaharamishwa. “Muda wa kujadili kwa pamoja matatizo yanayowakabili ndio huu. Mnajua namna Polisi na Mahakama vinavyowabana na kwamba mnahitaji kupata huduma nzuri

Mpango kuhusu Mali watayarishwa

Viongozi wa Afrika Magharibi wanatarajiwa kukutana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, kukamilisha mipango ya kuwatuma wanajeshi kaskazini mwa Mali. Mazungumzo hayo yatashughulika na mapendekezo ya kutuma wanajeshi elfu kadha kuwaondoa wapiganaji wa Kiislamu, iwapo juhudi za kufanya majadiliano hazitafanikiwa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limewasihi viongozi Afrika magharibi kutayarisha mpango huo kufikia mwisho wa mwezi huu. Mataifa ya Magharibi yamejitolea kutuma vikosi vya kutoa mafunzo kwa majeshi ya Afrika Magharibi.

HUYU NDIE ANASEMA SIASA ZA WAZIRI MEMBE NI ZA KINAFIKI, ANAFANYA MCHEZO WA KIHUNI NA ANAHUSIKA KUMCHAFUA RAIS KIKWETE

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi CCM, HUSSEIN BASHE Mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa wa CCM Hussein Bashe amefikia hatua hiyo ya kumtaja Benarnd Membe kutokana na vipeperushi vinavyodaiwa kusambazwa Dodoma kwamba Bashe na kundi lake limepanga kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu kupiga kura za maruhani ili Rais Kikwete asiwe na uongozi wa kofia mbili ikiwemo ile ya Uenyekiti wa Taifa wa CCM. BASHE amesema kwa mfumo wa kiuongozi ndani ya CCM ni mwendawazimu pekee anayewaza kwamba suala hilo linawezekana na kwamba kauli iliyotolewa na mmoja wa kada wa chama hicho AGUSTINO MATEFU juu ya kumpunguzia kura rais ni mkakati uliopangwa ili kumdhalilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa. Ili kuondoa utata wa juu ya anayehusika kuwatuma vijana wanaoeneza chuki na makundi ndani ya CCM, Bashe amemtaja mmoja wa Mawaziri wa awamu ya hii kwamba anaendesha mchezo mchafu ili kujisafishia njia ya Urais 2015. Wakati hayo yakitokea tayari maandalizi ya shughuli za ufunguz

LORD EYEZ AZUNGUMZA NA WAAANDISHI WA HABARI KUHUSU KESI INAYOMKABILI

Lord Eyez (kulia) akiwa na wakili wake wakati wakiongea na waandishi wa habari Mweusi toka A- City, Lord Eyez amekutana na waandishi wa habari akiwa na wakili wake ili kuzungumzia kesi inayomkabiri ya wizi wa vifaa vya gari ambayo ili-make headlines sana siku kadhaa zilizopita. Lord eyez amesema yeye kwa sasa anaiachia mahakama ambayo ndiyo itaweza kuchukua maamuzi ya kisheria kama yeye alihusika ama hakuhusika katika wizi huo wa vifaa vya gari. Wakili wa msanii huyo anayejulikana kwa jina la Peter Kibatala amesema kesi hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye ndiye mhusika wa wizi wa vifaa hivyo lakini kwa sasa hivi wanaiachia kwanza mahakama ndiyo itakayoweza kuchukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi hiyo. Hizi kauli za mweusi huyu na wakili wake zinaonekana zimepimwa na ruler ya kisheria kwa sababu ni kosa kisheria kujadili kesi ambayo iko mahakamani (commenting on a pending case). Weusi nao walisema ‘neno’ kuhusu tuhuma zinazomkabili

Wachimba migodi bado wagoma

Maelfu ya wachimba migodi wa Afrika Kusini wamekataa kurejea kazini, katika kampuni ya dhahabu nyeupe kubwa kabisa duniani iitwayo Anglo American, Amplats Taarifa zinazohusiana Afrika Kusini , Uchumi Wachimba migodi wanasema hawakubali pendekezo la kampuni hiyo kuhusu malipo. Mwezi Oktoba Amplats iliwafukuza makazini wachimba migodi 12,000 kwa sababu walishiriki kwenye mgomo katika migodi ya Rustenberg. Tangu wakati huo uchimbaji wa dhahabu nyeupe umeathirika sana. Amplats ni kampuni kubwa ya mwisho ya Afrika Kusini ambayo bado inaathirika na migomo - migomo iliyokuwa na ghasia ambapo watu zaidi ya 50 wamekufa. Wachimba migodi 34 walipigwa risasi na polisi katika mgodi wa kampuni ya Lonmin mwezi wa Agosti.

Photos-EBSS Waliohudhuria

Baadhi ya wadau, fans, ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa muziki wa Tanzania waliohudhuria fainali ya jana ya EBSS 2012.